WAKULIMA MKOANI GEITA WAHAMASIKA KULIMA KISASA NA KAMPUNI YA AGRICS.
Hata hivyo kampuni hiyo
imeendelea kuwasisitiza wakulima ambao hawajajisajili katika mradi kufanya hivyo
mapema kwani wakati unayoyoma.
Fursa hii ya mkopo wa mbegu za mahindi, alizeti,
mbolea ya kisasa, na sola kwa ajili ya mwanga kwa mkopo nafuu kabisa inalenga
kuwainua wakulima na kuwafanya wahame katika kilimo cha mazoea na kufanya
kilimo biashara.
Akiongea kwa niaba ya
kampuni hiyo Mratibu wa kampuni mkoa wa Geita Bwana Semeni Kime amewashukuru
wananchi kwa kuchangamkia fursa hiyo na pia amewataka waendeleee kujiunga kwa
wingi kwani hii ni fursa ya kipekee kwa maendeleo ya mkulima.
Pia amewatoa hofu wakulima
wa Geita juu soko la zao la alizeti kwani Agrics itashirikiana na kampuni dada
iitwayo Alizetics kununua alizeti ili kuwakikishishia soko la zao hilo.
Usajili utafika tamati mwezi
wa sita mwishoni hivyo wakulima wanaombwa kuchukua hatua za maksudi kuhakikisha
maendeleo ya mkulima na Geita kwa ujumla yanasonga mbele.
Semen Kime-Mratibu wa kampuni (Agrics) mkoa wa Geita
Post a Comment