Header Ads

Soko la Kayanga wilayani Karagwe laungua moto, Zimamoto watoka Bukoba kuzima moto



Soko la Kayanga wilaya ya Karagwe limeungua lote. Zimamoto kutoka Bukoba mjini ndio wamefika na kuanza kuzima moto.

- Moto umedhibitiwa kwa ushirikiano wa fire kutoka Bukoba na Kiwanda cha Sukari Kagera. Moto ulikuwa umeanza kusambaa kwenye maduka jirani na soko hilo.

Maoni yangu:

Haya ni masikitiko makubwa kwa viongozi wa wilaya kubwa kama hii kukosa gari la zima moto na vifaa vingine vya uokozi.Inabidi tufike sehemu serikali nayo iache kupendelea baadhi ya mikoa.Mikoa na wilaya zote zina wananchi wanaohitaji huduma sawa.

Sasa ona wilaya inakosa gari la zima moto wakati mkoa mwingine kuna magari mpaka taabu japokuwa nayo magumashi.

Poleni sana ndugu zangu wanyambo, nalikumbuka soko letu.

HABARI NA: THE CHOICE

No comments