MTI WAJERUHI WANAFUNZI WAWILI NA KUUA MMOJA WILAYANI BUKOMBE MKOANI GEITA
Wanafunzi watatu wakike wa Shule ya Sekondari Msasa iliyoko Kata ya Runzewe Mashariki wilayani Bukombe mkoani Geita jana wamepondwa na mti wakiwa Shuleni na kati yao mmoja amefariki dunia na wenzake wawili kujeruhiwa ambapo wamelazwa katika kituo cha afya cha Uyovu mkoani hapa
Kwa mujibu wa mkuu wa shule hiyo Mwl.Mokili Sagama amemtaja aliyefariki Dunia kuwa ni jackline bahati umri miaka 14 kutoka kijiji cha Nampangwe alikuwa akisoma shuleni hapo kidato cha pili.
Pia amewataja majeruhi wawili kuwa ni Eva Yohana kutoka kijiji cha Msangila na mwenzake Emiliana Elias kutoka kijiji cha musasa wote ni wanafunzi wa kidato cha pili.
Aidha kamanda wa polisi mkoani hapa Mponjoli mwabulambo alisema kuwa ni kweli jeshi la polisi linatambua kutokea kwa tukio hilo.
Post a Comment