WATU WATANO WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI
Baadhi ya wachimbaji wakifanya jitihada za kuokoa watu waliofukiwa na kifusi huko Mgusu mkoani Geita |
Watu watano wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa vibaya baada ya kuangukiwa na kifusi wakati walipokuwa kwenye shughuli za uchimbaji madini katika kata ya Mgusu wilayani na mkoani Geita.
Tukio hilo limetokea jana mnamo majira ya saa tisa alasili ambapo wachimbaji hao walifukiwa pindi walipo kuwa katika shughuli hiyo.
Akithibitisha kupokea miili hiyo mganga mfawidhi wa hospitali teule ya rufaa mkoani hapa bw, Adamu Sijaona amesema walio poteza maisha ni pamoja na Kazimili Seni umri miaka 55,Eva Moshi Maduhu umri miaka 23,Washima Makonda umri miaka 44,Shija Solo umri miaka 46 na Bahati Sipringi umri miaka 35 lakini kwa upande wa majeruhi ni Mboke Upepu umri miaka 30,Nkwimba Semi umri mika 54,Saimoni Jonathani umri miaka 23
Aliongeza kuwa majeruhi hao wamevunjika baadhi ya viungo vya mwili pindi walipo fukiwa na kifusi.
Baadhi ya wakazi walio shuhudia tukio hilo wamesema kuwa eneo hilo lilikuwa limezuiwa lakini baadhi ya watu walikaidi na wakawa wana ingia kuchimba pasipo kuruhusiwa ,hata hawa walio poteza maisha walitumia njia za kinyemela kuingia katika eneo hilo.
Kwa upande wake bw,Msimu Kabasa ambae ni fundi sanifu migodi ofisi ya madini Geita amesema kuwa hapo awali serikali ilitoa taarifa ya kuzuia shughuli za uchimbaji lakini baadhi ya wachimbaji walikaidi agizo hilo.
Bw,Kabasa alitoa kauli ya kulifungia eneo hilo kwa muda usiojulikana hadi pale serikali itakapo jirizisha kwa uchunguzi zaidi.
Aidha kaimu afisa madini wa wilaya ya Geita bw Fabiani Lukas alifika katika eneo la tukio nakusema kuwa tatizo kubwa la wananchi wamekuwa hawatii maagizo ambayo yana tolewa na serikali kwani eneo hilo walilizuia tangu awali kwasababu lilikuwa hatarishi lakini wachimbaji hawakutaka kutii agizo hilo ambapo pia amewataka wananchi kwa ujumla wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji kuwa na tabia ya kuwasikiliza viongozi wao pindi watoapo maagizo.
Post a Comment