KIKONGWE AUAWA KWA KUPIGWA NA JEMBE KICHWANI GEITA.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Lotson Mponjoli
Mama mmoja mkazi wa kijiji cha IKANDILO,kata ya Nyaruyeye ,Tarafa ya Busanda wilaya na mkoa wa Geita ameuawa kwa kupigwa na jembe lenye mpini kichwani,kwenye paji la uso na mdomoni na mtu asiyejulikana.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Geita Lotson Mponjoli amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi tarehe 29/02/2016 majira ya saa 6 usiku katika kijiji cha Ikandilo na kumtaja aliyeuawa kuwa ni MARIA D. MASHIMBI (78),msukuma na mkulima mkazi wa kijiji hicho cha Ikandilo.
Kamanda Mponjoli akielezea tukio hilo amesema kuwa siku ya tukio Maria alikuwa nyumbani na mumewe aitwaye COSMAS MAKIA (79) ambapo siku hiyo alifika mwanamme mmoja asiyefahamika nyumbani hapo na kuomba maji ya kunywa baada ya kupewa ndipo alipochukua jembe lililokuwa nje ya nyumba yao na kumpiga nalo marehemu kichwani akaanguka na kupoteza fahamu,kisha kushambuliwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso na mdomoni.
Mume wa marehemu alijaribu kumsaidia bila mafanikio.Kiini inaelezwa kuwa ni mgogoro wa shamba.
Tayari jeshi la polisi mkoani Geita linamshikilia mtu mmoja Jamanne Zabroni (54),mkulima mkazi wa Ikandilo kwa mahojiano zaidi kuhusiana na mauaji hayo.
HABARI NA:MRISHO SADICK
Post a Comment