Header Ads

Kesi dhidi ya Rushwa watumishi wa halmashauri ya Maswa kuisababishia hasara serikali kiasi cha milioni 4.7

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilaya ya maswa leo imewafikisha mahakamani watumishi wawili wa halmashauri ya wilaya ya Maswa kwa makosa matano ya kuisababishia hasara serikali kiasi cha shilingi milioni 4.7 kwa matumizi mbalimbali za nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya  mwajiri wao.

Akiwasomea mashitaka mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya maswa tumaini marwa ,mwendesha mashitaka wa takukuru mzalendo widege akiiwakilisha jamhuri ameiambia mahakama kuwa washitakiwa  hao wawili ambao wanashitakiwa kwa makosa matano ya kuhujumu uchumi ambao amewataja kuwa ni sostenes mazura afisa afya wa wilaya ya maswa na gundelina simbila  mhasibu idara ya afya ambaye alihamishiwa halmashauri ya kondoa wanashitakiwa kwa makosa matano.

Widege ameiambia mahakama kuwa washitakiwa hao wanashitakiwa kwa kosa la kwanza la kula njama wakiwa katika ofisi za halmashauri ya maswa mwaka 2013 kwa kutenda makosa ya lengo la kumdanganya  mwajiri wao .

Kosa la kwanza wote kwa pamoja walikula njama kifungu namba 32 cha sheria ya kuzuia   ya  rushwa ya 2007ambapo 24,mei ,2013 chini ya sheria namba 11ya 2007 walitumia  nyaraka ya kumdanganya mwanjiri stakabadhi  yenye namba 01224 kwa kmlipa bw frank mnenei kwaajili ya malipo ya kudurufu maandishi .

Mwendesha mashitaka ameendelea kuiambia mahakama kuwa kosa la tatu 29 january ,2013 kinyume na kifungu namba 22 walitumia stakabadhi namba 0351 ikiwa na maelezo ya kulipa gharama ya ukumbi wa mikutano wa  hotel ya ms kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano.

Katika kosa la nne watuhumiwa hao wanashitakiwa February 7,2013 walitumia stakabadhi namba  9675 na kuilipa kamupni ya prince kiasi cha milioni mbili na laki tano. Na kosa la mwisho la kuisababishia hasara serikali kiasi cha shilingi milioni 4.7 ambapo washitakiwa wote wamekana mashitaka na wako nje ya dhamana ambapo kesi hiyo itajwa tena machi 10 na itasikilizwa april 4,2016.

No comments