WAKAZI WA NYAKABALE WAMLALAMIKIA MKUU WA WILAYA KUWAITA WAHAMIAJI.
Wakazi wa Kijiji
cha Nyakabale kata ya mgusu,wamemlalamikia mkuu wa wilaya ya Geita,Manzie Omary
Manguchie kwa kuwaita wao ni wahamiaji
haramu.
Wakizungumza
na PAUL BAHEBE katika kijiji hicho wamesema kuwa swala ambalo amelifanya mkuu
wa wilaya si jambo zuri wala la busara
kwa kuwaita jina la wahamiaji haramu jambo ambalo limewakela na kuwauma.
Aidha kwa
upande wake diwani wa kata ya Mgusu Pastori Ruhusa ,amemwomba mkuu wa wilaya
kuacha tabia ya kutoa matamshi yasiyofaa kwa wananchi wake.
Kwa upande
wake mkuu wa wilaya ya Geita,Manzie Manguchie,amekanusha kuwaita majina hayo.
BONYEZA HAPA
CHINI KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WANANCHI HAO,DIWANI PAMOJA NA MAJIBU YA MKUU WA
WILAYA.
Post a Comment