WAKAZI WA MKOA WA GEITA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA.
Naibu waziri wa ardhi ,nyumba na manendeleo ya makazi,Mh,Angelina Mabula.
Wananchi mkoani Geita wametakiwa kuchangamkia fursa katika maeneo ambayo yameshatengwa na serikali ikiwa ni pamoja na kupanga au kununua nyumba za shirika la nyumba la taifa zilizopo katika kata ya bomba mbili Mkoani hapa.
Rai hiyo imetolewa na Naibu waziri wa ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi,Mh,Angelina Mabula katika ziara yake ya siku moja Geita, ambapo amesema kuwa kutokana na mji wa Geita kukua kwa kasi kubwa ni vyema wananchi kutumia fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na kuchukua maeneo yaliyowazi kwa ajili ya makazi.
Aidha kwa upande wake meneja wa kanda mwandisi,Benedict Kilimba,amesema kuwa mradi na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu unaendeshwa kutoka mkoa wa Mwanza kwa wilaya ya Geita na wilaya ya chato unaendeshwa kwa kupitia mkoa wa kagera.
Post a Comment