UPENDO NKONE AUNGANA NA ROSE MUHANDO NA MWAITEGE
Mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili hapa nchini, Upendo Nkone pia amethibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi mwaka huu katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama Nkone ameungana na wenzake waliothibitisha kushiriki tamasha hilo, Rose Muhando na Bonny Mwaitege tayari wamethibitisha wiki iliyopita.
Msama alisema hivi sasa kamati yake inaendelea na mchakato wa maandalizi ya tamasha hilo ambalo linatarajia kuanzia Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28).
"Tunaendelea na mchakato wa kufanikisha Tamasha la Pasaka 2016 ambalo litakuwa ni la aina yake kwa sababu linatarajia kutoa ujumbe wa Neno la Mungu kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa hasa kuhusiana na mauaji ya walemavu wa ngozi 'albino'," alisema Msama.
Aidha Msama alisema Tamasha la Pasaka lina malengo ya kufanikisha kuwasaidia wenye uhitaji maalum ambao ni pamoja na yatima na walemavu ambao husaidiwa kupitia tamasha hilo.
Msama alitumia fursa hiyo kuwataka wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kufanikisha matakwa ya wenye uhitaji maalum.
Post a Comment