Header Ads

MAJIBU YA MALINZI BAADA YA KUHUSISHWA NA UPANGAJI MATOKEO LIGI DARAJA LA KWANZA (Video)

Suala la timu za Geita Gold Sports, Polisi Tabora, JKT Oljoro na JKT Kanembwa leo limezua kizaa-zaa baada ya Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi kuulizwa swali na mmoja wa waandishi wa habari kwamba na yeye jina lake linatajwa kwenye harufu ya upangaji matokeo kwenye mechi za mwisho za timu hizo za ligi daraja la kwanza.
Swali hilo lilionekana kumuudhi Malinzi ambaye alilijibu swali hilo kwa hasira huku akionekana kukasirishwa kwa yeye kuhusishwa kwenye upangaji matokeo.
Swali aliloulizwa Malinzi: Moja kati ya watu wanaotajwa kuhusika na match fixing ni wewe mwenyewe Malinzi, inatajwa kwamba, wakati moja ya mechi inaendelea ulikuwa ukiwasiliana na mmoja wa msimamizi wa kituo ambaye ulikuwa unamtumia message baadaye alikamatwa. Je suala hili limekaa vipi?
Jibu la Malinzi: “Mimi sitaki ujinga, ‘I don’t want stupidity’ mimi ni mtu mzima naendesha taasisi kubwa, mwambie huyo mtu vituo vya polisi vipo. Match fixing ni kosa watu wamefungwa jela nchi nyingi mbalimbali na kama kuna mtu yeyote anaona kama Malinzi anausika katika huu ‘ushenzi’ aende akaripoti kituo cha polisi kilicho karibu na yeye tena aende leo”.
Malinzi amesema anajua kwamba watu wanaongea mengi kuhusu suala hilo na amekuwa akizungumzwa vibaya kwenye vyombo vya habari na hata kwenye mitandao ya kijamii.
Timu hizo zinahisiwa kupanga matokeo kutokana na matokeo ya mechi zao za mwisho kuwa na magoli mengi huku timu mbili za Geita Gold na Polisi Tabora ambazo zinawania nafasi ya kupanda ligi kuu zikishinda kwa idadi kubwa ya magoli.
Geita Gold na Poili Tabora zilikuwa zinalingana kwa kila kitu hivyo tofauti ya mabao ndiyo ingeamua ni timu ipi ningepanda ligi kuu. Kitu hicho kilipelekea timu hizo kushinda michezo yao ya mwisho kwa idadi kubwa ya magoli. Geita Gold ilishinda kwa bao 8-0 huku Poilisi Tabora ikishinda kwa bao 7-0.
Angalia video Malinzi alivyogeuka mbogo baada ya jina lake kuhusishwa na upangaji matokeo ya ligi daraja la kwanza.

No comments