Header Ads

JE WAJUA!!HII NDIYO IDADI YA MADHEHEBU YA KIKRISTO DUNIANI KOTE

Kwa mujibu wa historia imani ya waamini katika kristo ilianza mwanzoni kabisa mwa karne ya kwanza baada ya wakati wa kawaida kuanza kuhesabiwa.

Wakati huo imani hii ilifahamika kwa imani ya wagalilaya ambayo bado ipo huko katika nchi ya Israel katika kabila ya wayahudi.

Mara baada ya kuja kwa Kristo na kuzaliwa katika imani hii ya Wagalilaya,umaarufu wa dini hii ulipata kasi kubwa sana kutokana na matendo yaliyokuwa yakifanywa na Kristo Yesu.

Hadi kufa kwake imani hii bado ilikuwa ikifahamika kwa jina la imani ya kiyahudi,kabla ambapo jina hili lilipokuja kubadilika na kufahamika kama imani ya waamini katika Kristo,ambapo inasemekana ilianza mara baada ya Yesu kupaa juu mbinguni mara baada ya kufufuka kutoka kaburini.

Mengi yanafahamika juu ya imani hii na waamini wake juu ya namna wanavyoabudu na kusali kupitia kwa Yesu Kristo.

Lakini JE WAJUA kuwa hadi kufikia sasa kuna jumla ya madhehebu 33830 yanayotambulikana kama waamini wa imani kaika Kristo Yesu?

Ndiyo hii ndivyo ilivyo ambapo jumla hii inaifanya imani ya Kikristo kuwa na madhehebu mengi zaidi kuliko imani yoyote ile duniani.

No comments