Chatu Aonekana Manispaa ya Songea, Wananci waingiwa na hofu.
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Matuli kata ya Majengo na Mfaranyaki makaburini manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wameingiwa na hofu ya usalama wa maisha yao baada ya kuonekana kwa Chatu ambaye anazunguka katika pori la mto unaotenganisha maeneo hayo
Nyoka huyo ameonekana Zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti,taarifa zilipoenea timu ya waandishi wa habari ilitembelea eneo hilo kuzungumza na wananchi juu ya hofu na mashaka waliyonayo wananchi hao wamesema toka wapate taarifa ya uwepo wa chatu shughuli za kilimo katika bonde la mto Ruvuma zimesimama na watoto wamezuiliwa kuchota maji.
Inadaiwa kuwa mbwa watatu wameliwa na chatu hivyo wananchi wameomba maafisa wanyama poli wafanye msako wa kumtafuta kabla hajaleta madhara kwa binadamu na kwamba wanamashaka kuwa wamezombwa na maji ya mvua kutoka milima ya Matogoro.
Taarifa ya kuonekana kwa chatu huyo imefikishwa kwenye ofisi a maliasili wanyama poli wilaya ya Songea wataalamu hao wameshafika eneo la tukio na kuwataka wananchi kufyeka nyasi maeneo ya nyumba zao na kutao taarifa mara moja anapoonekana kwani tabia yachatu akimeza mbwa anakaa Zaidi ya wiki moja eneo hilo bila kutoka.
Post a Comment