Header Ads

Watu Wanaosadikiwa Kuwa Majambazi Wakwama Kuiba Katika Mgodi Wilayani Geita.

Watu wanaodaiwa kuwa majambazi wamevamia mgodi Ibondo Januari 15 majira ya saa tano usiku kwa lengo la kuiba kaboni inayotumika katika shughuli za ukamataji wa dhahabu katika kijiji cha Nyarugusu Wilayani Geita.
Watu hao wanaodaiwa kuwa kumi na nne walifanikiwa kuingia katika Mgodi huo lakini kabla ya kutimiza azma yao ya kuiba walifanikiwa kukamatwa na kufikishwa katika kituo cha Polisi Kijijini hapo.
CREDIT:GEITA INFO

No comments