Header Ads

WALIOVUNJIWA NYUMBA WAANDAMANA DAR.

Jeshi la Polisi Jumatatu hii limezima ghasia za wananchi wenye hasira maeneo ya Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam baada ya kupinga zoezi la bomoa bomoa kwa mara ya pili kufuatia kukataa kuondoka katika eneo hilo kwa madai hawana pa kwenda.

Akizungumza na mtandao huu Jumatatu hii mmoja kati ya waathirika wa bomoa bomoa hiyo, Bi Fatuma Said, amesema wanashindwa kuondoka katika eneo hilo kwa kuwa hawana sehemu ya kwenda huku akiitaka serikali kuwafikiria.

“Sio kwamba tumegoma kuondoka wengine sisi hatuna sehemu ya kwenda,” alisema. 
“Sisi baada ya kubomolewa nyumba yetu tukashindwa kuondoka kwa kukosa pa kwenda.Tukaamua kujenga hapa vijibanda ili serikali itufikirie lakini tunashangaa leo asubuhi vibanda vyetu vimewekwa X kwamba wanataka kubomoa. Saa tano tumeingiliwa kwenye vibanda vyetu sisi tukakimbia wao wakachoma ndio baadhi ya wanacnhi wakaingiwa na hasira na kwenda kuchoma matairi barabarani,”alieleza.
 
Hadi sasa polisi wanawashikilia vijana kadhaa wanaohusishwa na tukio hilo.

==> Hapa Chini Kuna Video Ya Tukio Hilo. Itazame Ujionee

CREDIT:Mpekuzi blog

No comments