Wachimbaji Wadogo bado wana Kilio cha Kukosa Maeneo ya Uchimbaji.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dokta Medard Karemani ametoa siku kumi na nne kwa mgodi wa Buckreef kuanza uzalishaji wa dhahabu na kama wakishindwa kutimiza sharti basi Serikali itachukua eneo hilo.
Hatua hiyo imekuja baada ya muda mfupi kuwatembelea wachimbaji wadogo eneo la Lwamgasa na kulalamika juu ya mgodi wa Buckreef kuhodhi eneo kubwa bila ya kulifanyia shughuli na kuwaacha wachimbaji bila maeneo.
Post a Comment