Nape Nnauye: Kasi Ya Rais Magufuli Itaviua Vyama Vya Upinzani Hapa Nchini
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kasi ya utendaji kazi ya Rais John Magufuli inaweza kuua uwepo wa vyama vya upinzani nchini.
Hata hivyo alisema kuwa hangependa upinzani ufe kwa vile hiyo pia itakuwa imeua demokrasia nchini na kudai kuwa lengo la kuanzisha vyama vya siasa haikuwa kuviua bali ni kuviona vikiendelea kuwepo.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu huyo wakati alipokuwa akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya miaka 39 ya CCM ambayo kilele chake kimepangwa kufanyika mkoani hapa Februari 6, mwaka huu badala ya Februari 5 iliyozoeleka.
Alisema kuwa chama kimelazimika kubadili tarehe ya kilele ili kuwawezesha wananchi kushiriki ipasavyo maadhimisho hayo kwa kufanya kazi badala ya kuwa na sherehe mbalimbali.
“Maadhimisho ya safari hii ni tofauti na ya miaka mingine. Safari hii wananchi watatakiwa kushiriki zaidi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo. Kauli mbiu yetu ni ‘Sasa kazi’ hivyo watu wafanye kazi ili wajiletee maendeleo yao wenyewe,” alisema.
Post a Comment