MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA MKOANI GEITA.
Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan jana jioni aliwasili mkoani Geita na akakutana na uongozi wa mkoa huo ambapo alisisitiza suala la wananchi kunufaika na mgodi wao wa dhahabu wa Geita Gold Mine.…
"Wakati nilipopita kwenye kampeni nilipita kwenye mgodi wa Geita Gold Mine nikaangalia hali ya watu wa Geita nikawa na majonzi makubwa…sikuridhika kuwa na mgodi mkubwa kama ule na hali ya watu wa Geita iko ilivyo hivi nikawa sikuridhika nilikuwa mkali kidogo." Alisema Mama Samia na kuongeza;
"Wakati naangalia presentation nimeona amount nzuri kidogo inatolewa kwenda kwa watu ingawa bado ninamaswali yangu ambayo nitayafanyia kazi ili tuone ni kiasi gani sahihi kinatakiwa kutolewa na mgodi kwenda kwa wananchi, dhahabu iliyopo niyawana Geita Mungu amewaumbia katika ardhi yao
"Hatukatai kuwa na wawekezaji wachimbe lakini uchimbaji uwe na faida kote wao wapate na wananchi wapate kwa hiyo hatunabudi kusimamia vizuri na kuhakika kwamba wananchi wa Geita wanafaidika na rasilamali ambayo Mwenyezi Mungu amewapangia."
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa GGM Mkoani Geita jana Januari 04,2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wawekezaji wa Mgodi wa GGM Mkoani Geita alipowasili Uwanja wa ndege wa GGM Geita jana Januari 04, 2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa akizungumza wakati akitoa Taarifa ya Maendeleo ya Mkoa wa Geita, kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia), katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, jana Januari 4, 2016. Katikati ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Injiani Gerson Lwenge.
Post a Comment