Header Ads

WANAODHURUMU WALENGWA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI KUKIONA.


Mratibu wa Tasaf Wilayani Mbogwe mkoani  Geita Mercy Joseph amewaonya watendaji , mabalozi na wenyeviti  wa vijiji na wale wote wanaofanya mchezo wa kuwadhurumu walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini baada ya kupokea msaada huo wao wanawatoza ushuru wakibainika watachukuliwa hatua kali.

Onyo hilo Mercy amelitoa baada ya Mbunge wa jimbo la Mbogwe Agustino Masele kuyafikisha malalamiko ya wananchi ofisini kwake kuwa wapo watu wanaowaomba walengwa fedha  za ushuru kwa kuwa waliwasaidia majina yao kukubaliwa.

Amesema  baada ya kusikia kauli hiyo toka kwa mbuge kuwa kuna watu wanafanya
Mchezo huo  ameamua kupita kila kijiji kuwaelimisha tena walengwa kuwa wasikubali kumpatia mtu yeyote fedha hizo ambazo wanapokea kila baada ya wiki mbili na hivyo kama kuna mtu anafanya hivyo huyo ni mwizi hivyo amewataka wamtajie majina  ya watu hao ili awachukulie hatua.

Joyce Peter ni mkazi wa kijiji cha Shinyanga B amesema kuwa kweli wanafanyiwa hivyo kwa lengo la kwamba  waendelee kusaidiwa ili majina yao  yasije yakafutwa na  kukakosa msaada



Mratibu  wa Tasaf  ameongeza kuwa  kila anapopita vijijini wananchi wamekuwa waoga kuwataja wale wanaowafanyia vitendo hivyo kwa kile alichobaini kuwa huenda wakiwataja basi wanaweza kufanyiwa kitu chochote hivyo ametoa simu yake kwa walengwa wote waliochaguliwa kwenye uhawilishaji na majina yao yameshaanza kupokea fedha ili waweze kumtumia  majina.

HABARI NA PETER MAKUNGU VIA JOEL MADUKA PEKUZI ZA MTAA.

No comments