Header Ads

Waislamu wagawa maua Washington, waonesha Uislamu ni dini ya upendo.


Waislamu mjini Washington Marekani wamegawa maua kwa watu wa dini na mataifa tofauti ili kuonesha kuwa Uislamu ni dini ya amani na upendo na wakati huo huo kupambana na propaganda za kueneza chuki dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu katika nchi za Magharibi ikiwemo Marekani.
Mwandishi wa Press TV ameripoti habari hiyo kutoka mjini Washington Marekani na kuongeza kuwa, Waislamu hao wamechukua hatua hiyo katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Nabii Isa AS kwa mujibu wa imani ya Wakristo.
Wanaharakati wa Kiislamu mjini Washington wamesema kuwa wameongeza jitihada za kuhubiri amani na mapenzi kwa watu wa matabaka na mataifa tofauti nchini Marekani.
Waislamu wanaoshiriki kwenye mpango huo wameongeza kuwa, Waislamu ni watu wanaopenda amani na utulivu na ni watu wanaopinga dhulma ya aina yoyote ile.
Hatua ya Waislamu hao imepokewa vizuri na wananchi wengine wa Marekani.
Baada ya kutokea shambulio la kigaidi mjini Paris Ufaransa hivi karibuni, Waislamu wa maeneo tofauti ya Marekani wameongeza kampeni zao za kutangaza mafundisho sahihi ya Uislamu na kuwaonesha walimwengu kuwa Uislamu haukubaliani hata chembe na vitendo vya kigaidi.
CHANZO:IRAN SWAHILI

No comments