MTOTO AFANYIWA UKATILI NA JIRANI KISA TV.
Mtoto Sabrina akiwa na majeraha usoni baada ya kumwagiwa maji ya moto na jirani kisa TV.
Na Makongoro Oging’
UBINADAMU umeisha! Ni ajabu lakini ni kweli imetokea! Mtoto Sabrina (7), mkazi wa Tabata Msimbazi, Dar anakabiliwa na maumivu makali kufuatia majeraha yaliyotokana na kumwagiwa maji ya moto na mwanamke anayesemekana ni jirani yao.
Tukio hilo la kushangaza lilijiri saa sita mchana wa Desemba 6, mwaka huu wakati mtoto huyo alipokuwa akiangalia kupitia dirishani, kipindi cha watoto kilichokuwa hewani runingani katika nyumba ya jirani yao huyo (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye hapendi watoto wa majirani zake waende kwake.
Akizungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita nyumbani kwake, Tabata jijini Dar, mama mzazi wa mtoto huyo, Mariam Athuman alisema siku ya tukio, Sabrina alikuwa akicheza nje ya nyumba kisha akaenda kwa jirani huyo kuangalia kipindi cha watoto.
“Nikiwa nyumbani, alikuja mtoto mmoja akaniambia Sabrina amemwagiwa maji ya moto akiangalia tivii kwa jirani. Inasemekana mara ya kwanza alianza kumwagiwa maji ya baridi, akakimbia lakini baadaye akarudi tena.
“Huyo mtoto aliyeleta taarifa alisema mtu aliyefanya unyama huo aliagizwa na shangazi yake ambaye anaishi naye. Alipewa maji ya moto, akaambiwa ammwagie usoni Sabrina.
“Wakati naelekea eneo la tukio nilikutana na mwanangu akitembea kwa shida. Alikuwa haoni vizuri huku amebabuka uso. Nilimkimbiza kwenye Zahanati ya Tabata ambako walimsafisha uso kwa dawa kisha wakaniandikia nyingine za kununua.
“Baada ya hapo, nikaenda Kituo Kidogo cha Polisi Tabata. Pale nilifungua kesi kwa jalada namba TBT/RB/7418/2015 na jalada la uchunguzi TBT/IB/3835/2015.
“Polisi walimfuata aliyedaiwa kutumwa na shangazi yake ambapo alikiri kufanya tukio hilo. Polisi walimfuata shangazi huyo na kumchukua hadi kituoni, akawekwa mahabusu, mimi nikaondoka.
“Cha ajabu ni kwamba, baada ya kufika nyumbani, kama dakika ishirini mbele, nilimwona mtuhumiwa na shangazi yake wamerudi. Hatukujua sababu ya kuachiwa mapema kiasi hicho. Hii dunia ni katili sana,” alisema mama huyo huku akitokwa machozi.
Wakazi wa eneo hilo wameiomba serikali imchukulie hatua kali mwanamke huyo aliyetoa maagizo ya kufanyika kwa ukatili huo.
Uwazi lilifika kituo hicho cha polisi na kuuliza kisa mtoto huyo kuchomwa kwa maji ya moto lakini hakuna askari aliyekuwa tayari kutoa ushirikiano kuhusu kuachiwa kwa mtuhumiwa muda huohuo kama mlalamikaji alivyosema huku mkuu wa kituo akisemekana kuwa nje ya kituo.
Na Makongoro Oging’
UBINADAMU umeisha! Ni ajabu lakini ni kweli imetokea! Mtoto Sabrina (7), mkazi wa Tabata Msimbazi, Dar anakabiliwa na maumivu makali kufuatia majeraha yaliyotokana na kumwagiwa maji ya moto na mwanamke anayesemekana ni jirani yao.
Tukio hilo la kushangaza lilijiri saa sita mchana wa Desemba 6, mwaka huu wakati mtoto huyo alipokuwa akiangalia kupitia dirishani, kipindi cha watoto kilichokuwa hewani runingani katika nyumba ya jirani yao huyo (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye hapendi watoto wa majirani zake waende kwake.
Akizungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita nyumbani kwake, Tabata jijini Dar, mama mzazi wa mtoto huyo, Mariam Athuman alisema siku ya tukio, Sabrina alikuwa akicheza nje ya nyumba kisha akaenda kwa jirani huyo kuangalia kipindi cha watoto.
Sabrina akiwa na mama yake mzazi

Post a Comment