Mama Diamond, Wolper Wafunika Kwenye Video ya Je Utanipenda?
Kuna msemo usemao “experience is the best teacher”, msemo huu umekamilika kupitia mama mzazi wa msanii Diamond Platnums , baada ya kuigiza kama mama ambaye ana maisha magumu kupitiliza,huku akiwa ameuvaa uhusika vilivyo kupitia video mpya ya msanii huyo ambaye ni mwanae wa kumzaa huitwao, je utanipenda.
Mama diamond, ni kati ya watu wachache waliotumika kwenye video hiyo na kuifanya ionekane kuwa na mvuto wa kipekee na kubeba hisia za mamilioni ya watanzania kwa uchezaji wa hali ya juu alioonyesha kwenye video hiyo.
Mbali na mama diamond, msanii wolper nae anatajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine kuifanya video hiyo kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na uchezaji wake wa nyodo na dharau,hulka iliyomvaa vilivyo na kuitendea haki.
Mashabiki wengi waliyoiona video hiyo wamempongeza sana mama diamond kwa kuvaa uhusika, na kumtabiria kufanya vyema kwenye sekta ya uigizaji kama akiamua kuingia huko.
Warumi-JF
Post a Comment