Header Ads

KANISA LA E.A.G.T KANDA YA ZIWA MAGHARIBI LAFANYA UCHAGUZI.

  • Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania(E.A.G.T) kanda ya ziwa magharibi leo limefanya uchaguzi kuchagua viongozi wa majimbo na kanda ambapo aliyechaguliwa kuwa Askofu wa kanda hiyo ni Mchungaji Machimu toka Shinyanga na makamu wake ni Mchungaji Joshua Wawa kutoka kanisa la E.A.G.T Migombani Sengerema.Kwa upande wa majimbo jimbo la Geita Askofu aliyechaguliwa ni Zacharia Seni,makamu wake ni Ibrahim (majembe),Katibu ni Mch.Robert Ngai na Mhasibu Silva Mjogo.
Jimbo la Shinyanga Askofu ni Marco Ngule,Jimbo la Biharamulo Askofu ni Paul Bonifasi,Makamu Lukas Francis na katibu Sospeter Gaula,Jimbo la Bukombe Askofu ni Charles Paul makamu ni Richard Kazoba,Jimbo la Sengerema Askofu ni Jonathan Lutego,makamu Askofu ni Mch.Batondane.
Jimbo la kahama Askofu ni Bathlomayo Cheketela.Jimbo la Bukoba Askofu ni Alongino Kabakaki.

Aidha kutokana na ukubwa wa jimbo la Kagera,imelazimika kuzaliwa jimbo jipya la Karagwe ambalo hata hivyo wachungaji kutoka Karagwe walikuwa kumi kati ya wachungaji 68 wanaotokea Karagwe, hivyo ikamlazimu Askofu wa Kanda ya ziwa magharibi Mchungaji Machimu kuahirisha uchaguzi wa viongozi katika jimbo hilo jipya na kuwaahidi kuwa uongozi wa kanda utaenda huko kwa ajili ya kusimamia uchaguzi.
Uchaguzi huo umefanyika leo katika kanisa la E.A.G.T Ihayabuyaga Geita mjini kwa Mch.Ibrahimu Majembe makali na kuhudhuriwa na wachungaji mbalimbali wa E.A.G.T kutoka Mikoa ya Shinyanga,Geita,Kagera na Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Askofu mteule wa jimbo la Geita Zacharia Seni akiteta jambo na wachungaji nje ya kanisa la E.A.G.T Geita mjini.


Makamu Askofu wa kanda Joshua Wawa akiwa na wachungaji wengine nje ya kanisa la E.A.G.T Geita mjini.
      Makamu Askofu Joshua Wawa kulia akisikiliza jambo kwa makini kutoka kwa mmoja kati ya wachungaji waliohudhuria uchaguzi huo leo.


Askofu mteule jimbo la Sengerema Jonathan Lutego mwenye tai akiangalia jambo wakati wakisubiri kuingia kanisani kwa ajili ya kuendelea na uchaguzi.

Makamu Askofu wa jimbo la Sengerema Mch.Batondane  (kulia) akiwa na Askofu wa jimbo Geita Zacharia Seni.

Pongezi zikiendelea baada ya kuchaguliwa.


Mweka hazina wa jimbo Geita anayemaliza muda wake(kulia katikati) Mch.Metson Asheri akiteta jambo na wachungaji wenzake.



Zoezi la upigaji kura likiendelea.

Makamu Askofu jimbo la Sengerema Mchungaji Batondane akifuatilia zoezi la uchaguzi kanisani.

Safu ya uongozi jimbo la Geita ambayo imeachia ngazi rasmi na kukabidhi usukani kwa uongozi mpya.

Zoezi la kuhesabu kura likiendelea.

Askofu mteule jimbo la Sengerema Jonathani Lutego akitafakari jambo.

Askofu mteule jimbo la Biharamuro Paulo Bonifasi.

Makamu Askofu jimbo la Biharamulo Lukas Francis.

Askofu mteule jimbo la Geita Zacharia Seni(kulia)akiwa na Katibu wa jimbo hilo Mchungaji Robert Ngai ambaye ameweza kutetea kiti chake cha ukatibu kwa muhula wa pili sasa.

Askofu wa kanda ya ziwa magharibi Mchungaji Machimu akitoa maelekezo kwa wapiga kura.

Makamu Askofu jimbo la Geita Ibrahimu Majembe akiwa kanisani wakati zoezi la upigaji kura likiendelea.

Askofu mteule jimbo la Bukombe Charles Paul.

Katibu wa jimbo la Geita mteule Mchungaji Robert Ngai.

Mweka hazina mteule Silva Mjogo ambaye hapo kwanza alikuwa makamu Askofu jimbo la Geita.

Askofu mteule jimbo la Kahama Mchungaji Bathlomayo Cheketela.

Askofu mteule jimbo la Bukoba Alongino Kabakaki.

No comments