Header Ads

AGIZO LA MAGUFULI LAPOKELEWA HATA MAKANISANI.



Agizo la Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli kuwa tarehe 9 Decemba ambayo ni maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika kila mwaka yafanyike kwa kufanya kazi hususani usafi ili kuepukana na magonjwa ya milipuko kama kipindupindu, agizo hilo limepokelewa na wananchi kwa moyo mmoja.
Leo PAULBAHEBE BLOG katika pita pita zake imeshuhudiwa waumini wa kanisa la E.A.G.T katundu-Geita lililo chini ya uongozi wa Mch. Robert Ngai wakihimizwa kufanya usafi kesho kutwa siku ya Jumanne katika eneo la kanisa na nyumbani kwa mchungaji kisha katika maeneo wanayoishi.
Hayo yamesemwa na Mzee wa Kanisa Donald Naset alipokuwa akitoa matangazo kanisani hapo na kuwasisitiza waumini kuwa usafi usiishie tu tarehe 9 kama agizo la Mh.Magufuli bali usafi iwe ni tabia yao ya kila siku" usafi ni kawaida yetu kwani Mungu wetu ni Mungu wa Usafi(utakatifu)" amesema.
Jumatatu ya tarehe 23/12/2015 taarifa rasmi ya Ikulu ilitolewa juu ya kufutwa kwa sherehe za uhuru disemba 9.

Kwa mujibu wa  Sheria ya Sikukuu za Kitaifa  (The Public Holidays Act, Cap 35) pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliamua kuwa maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika tarehe 9 Desemba, 2015, yatumike  kwa kufanya kazi.  
  
Kwamba maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu  (2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi (Uhuru na Kazi) katika Taifa letu.  
  
Mheshimiwa Rais alielekeza Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.
Akihubiri wakati wa neno mchungaji wa kanisa hilo Robert Ngai aliwakumbusha waumini hao juu ya "IBAADA INAYOMPENDEZA MUNGU"ambalo ndilo lilikuwa somo jumapili ya leo.
Nao waumini wa kanisa hilo wameeleza kufurahishwa na kasi ya Rais Magufuli na kuongeza kuwa wanaimani kuwa ataipeleka nchi katika uchumi ulio imara.

No comments