Header Ads

WALINZI WA G4S KATIKA MGODI WA GGM GEITA WAGOMA.


Habari na Joel Maduka.
Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi g4s mkoani geita wanaofanya kazi katika mgodi wa dhahabu wa GGM, wamelazimika kugoma leo kwa kile wanachodai ni kutokana na kuwepo kwa maslahi madogo na malipo duni katika kampuni  hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wafanya kazi wenzake,  pascal temba,amesema kuwa kuna mambo manne ambayo yamewalazimu kugoma ikiwa ni pamoja na kuwapo kwa uongozi mbaya, mazingira kuwa magumu wanayofanyia kazi na kupatiwa malipo duni ambayo hayaendani na mikataba waliyopatiwa.

 Aidha kwa upande wakeEvaryn Raiza,ambaye ni moja kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo,ameongeza kuwa mgomo huo utadumu endapo kama hautapatiwa ufumbuzi na kutatuliwa matatizo waliyonayo na yanayoendelea kuwasumbua kwa kipindi kirefu.

Mkuu wa wilaya ya Geita,Manzie Omary Mangochie,amemaliza mgomo huo kwa kuwataka wafanyakazi warejee kazini na serikali kupitia viongozi wa kampuni hiyo watahakikisha wanazungumza na kufikia makubaliano kwa yale ambayo wamekuwa wakiyadai kutimiziwa katika kazi  wanazozifanya.



Wafanyakazi wa g4s wamerejea kazini na kwamba kutaundwa kamati ambayo inatarajia kukutana kesho kwa ajili ya kuzungumza na mkuu wa wilaya kujua hatma na utatuzi wa madai ya wafanyakazi hao.

No comments