MBUNGE WA LUDEWA MH.DEO FILIKUNJOMBE AFARIKI DUNIA KWA AJALI.
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe amefariki dunia baada ya helikopta aliyokuwa akiitumia kwa ajili ya kampeni kupata ajali jana usiku.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na meya wa manispaa wa Ilala Jerry Slaa ambaye pia amempoteza baba yake kwenye ajali hiyo.
"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha", ameandika Slaa.
Ajali hiyo imetokea jana jioni ambapo Capt. William Silaa akiwa na mh.Deo Filikunjombe na abiria wengine walikuwa kwenye helikopta hiyo yenye namba 5Y-DKK wakitokea Dar kuelekea Ludewa.
Helikopta hiyo ilianguka kwenye msitu wa Selous.
Kwa taarifa zaidi tutaendelea kukuletea kuhusu tukio hili.
PAUL BAHEBE BLOG tunapenda kutoa pole kwa chama cha mapinduzi,watanzania na familia za wote waliofikwa na msiba huu mkubwa.
Post a Comment