Header Ads

MAFURIKO YA LOWASSA YAENDELEA GEITA.

Katika kuendelea na kampeni zake mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo mheshimiwa Edward Lowassa leo Jumanne ameendelea na kampeni zake mkoani Geita  katika majimbo matatu.
Akiwa katika jimbo la Geita mjini kwenye uwanja wa magereza mheshimiwa Lowassa amesisitiza kuwa jambo la kwanza atakaloanza nalo mara baada ya kuingia madarakani ni Elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya Elimu kuanzia awali mpaka chuo kikuu.
Kwa upande wake waziri mkuu mstaafu mh.Fredrick Sumaye amesema kuwa mabadiliko ni kuhakikisha kuwa wanatimiza na kutatua changamoto zilizopo nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha kwa watanzania,afya,maji pamoja na Elimu na kuhakikisha kuwa wanatatua tatizo la ajira kwa vijana.
Kesho jumatano mheshimiwa Lowassa anatarajiwa kuendelea na kampeni zake katika mkoa wa Kagera.
 Umati wa watu waliojitokeza kusikiliza sera za mgombea urais kupitia CHADEMA ambaye anaungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA mheshimiwa Edward Lowassa katika viwanja vya magereza.
 Mmoja kati ya wananchi aliwaacha watu midomo wazi baada ya kuja mkutanoni na mbuzi kwa ajili ya zawadi kwa mheshimiwa Lowassa.





 Mgombea wa urais kupitia chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa Edward Lowassa akiwapungia mkono wananchi wakati akiwasili katika viwanja vya magereza Geita mjini.
 Mmoja kati ya mashabiki na wanachama wa chadema Samson akitoa burudani uwanjani hapo kwa njia ya mashairi.


 Mheshimiwa Edward Lowassa akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Geita.
 Mgombea ubunge jimbo la Geita mjini Lodgers Luhega akielezea matatizo ya wanageita mbele ya Mgombea urais wa chama hicho Edward Lowassa.
Lowassa akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Geita mjini mheshimiwa Rodgers Luhega.

No comments