Wanataka kuufungia wimbo wangu mpya ‘Viva Roma viva’ kisa tu nimeongea ukweli – Roma.
Saa chache baada ya wimbo mpya wa Roma ‘Viva Roma viva’ kutoka September 9, rapper huyo amedai kuwa ametishiwa wimbo huo kufungiwa.
![roma new pic](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2015/09/roma-new-pic.jpg)
Kupitia Instagram, majira ya saa mbili usiku Roma aliandika;
“WANATAKA KUIFUNGIA NYIMBO YANGU!! KISA TU NIMEONGEA UKWELI!! INANIUMA SANA NATAMANI HATA KULIA NIKIONA UKWELI HAUPEWI NAFASI!! NIOMBEENI NA MNIKUMBUKE KWENYE SALA ZENU NDUGU ZANGU!! Viva Roma viva”
![ro](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2015/09/ro.jpg)
Bado haijafahamika sababu ya wimbo huo kutaka kufungiwa, na Roma hakupatikana kwenye simu yake nilipomtafuta kwaajili ya kuzungumza nae kuhusu swala hilo.
Post a Comment