Header Ads

PICHA:HALI HALISI YA GEITA PAMOJA NA KUWA NA UTAJIRI WA DHAHABU.


Geita ni moja kati ya maeneo tajiri sana hapa Tanzania kwa rasilimali za kutosha kama dhahabu,ni moja kati ya miji inayosifika sana,lakini kubwa zaidi ni moja kati ya miji masikini Tanzania.
Pamoja na utajiri uliopo katika mji wa Geita bado zipo changamoto nyingi zinazowakabili wananchi wa Wilaya na mkoa huu ikiwa ni pamoja na Maji,umeme kukatika hovyo tena bila taarifa,miundo mbinu mibovu na ya kuhuzunisha unaweza kulia ukilinganisha na utajiri uliopo,zao la pamba lililokuwa zao pekee wilayani hapa kutelekezwa na jineri za Kasamwa kugeuzwa kuwa makambi ya FFU. Wananchi wake kuwa ombaomba na masikini wa kutupwa kwa kukosa maeneo ya kuchimba wakidaiwa kuwa ni wavamizi.
Huduma za afya mbovu,upungufu wa dawa,na huduma mbovu,shule kukosa madawati na mengine mengi ambayo hayaelezeki.
Kinachonishangaza ni wagombea badala ya kuyazungumzia wamekalia vijembe majukwaani! kwa maoni yangu ni bora wakafungue bendi za taarabu.





 Hii ndio stendi ya magari ya kisasa iliyopo Geita mjini iliyogharimu mamilioni ya shilingi katika ujenzi wake hongera halmashauri ya Geita na wakandarasi kwa kazi nzuri.




 Hii ndio stendi ya magari ya kisasa iliyopo Geita mjini iliyogharimu mamilioni ya shilingi katika ujenzi wake hongera halmashauri ya Geita na wakandarasi kwa kazi nzuri.




No comments