Header Ads

MZEE AUAWA MOROGORO,AZIKWA KWENYE UVUNGU WA KITANDA.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul.
POLISI mkoani Morogoro inawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kufanya mauaji ya Pascal Luwi (70) , mkulima na mkazi wa Kitongoji cha Kombora Kijiji cha Ubiri Kata ya Mhonda Tarafa ya Turiani wilayani Mvomero na kumzika uvunguni mwa kitanda chumbani mwake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema mjini hapa jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 8:30 nchana katika kijiji cha Ubiri. Alisema, watuhumiwa hao wanadaiwa kumuua Luwi na baada ya kumuua waliuzika mwili wake chumbani kwake chini ya uvungu wa kitanda.
Kamanda Paulo aliwataja waliokamatwa kuhusu tukio hilo ni John Pascal Mndimbo (37), Fredrick Michael (45) , Mwajuma Pascal (36) na Anthony Kadudu . Kamanda alisema mzee huyo alitoweka nyumbani kwake Septemba 4, mwaka huu hadi Septemba 15, mwaka huu mwili wake ulipopatikana ukiwa umezikwa ndani ya nyumba yake .
Kamanda Paulo alisema marehemu alionekana kupigwa na kitu kizito kichwani na inaelezwa kiini cha mauaji hayo ni ugomvi wa shamba la ekari moja la mzee huyo lenye mazao ya hiliki na miwa, ambapo watoto walitaka wapewe shamba hilo kutoka kwa baba yao.

Alisema Polisi inawashikilia watu hao wanne kwa mahojiano kuhusu tukio hilo, akiwemo mtoto wa marehemu aitwaye Mwajuma Pascal. Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baaada ya upelelezi kukamilika.HABARI LEO

No comments