Header Ads

MAKANISA MATATU YACHOMWA MOTO BUKOBA.

1Kanisa lilivyoteketea kwa moto.
3
Kinanda kinchotumiwa na wanakwaya kwa ajili ya kupigia muziki kikiwa kimeungua.
4 5
Makanisa hayo baada ya kuteketezwa kwa moto.
6
Waumini wa makanisa hayo wakiwa wamekusanyika kushuhudia tukio hilo.
7
Mabaki ya kanisa baada ya kuteketezwa kwa moto.
8
Mmoja wa viongozi wa makanisa hayo akizungumza wa waandishi wa habari baada ya kukuta kanisa lake limechomwa moto.
WATU wasiojulikana wamechoma makanisa matatu mjini Bukoba jana. Makanisa yaliyochomwa moto ni Pentecostal Assemblies of God (PAG) eneo la Buyekera, Living Water International na Evangelical Assemblies of God (EAGT) kata ya Kibeta yote ya mjini Bukoba.
Wachungaji na viongozi wa kiroho wa makanisa hayo wametoa wito kwa vyombo vya dola kuwabaini wahusika wa tukio hilo linaloashiria  uvunjifu wa amani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augstine Oromi, amethbitisha kutokea kwa tukio hilo  na kusema kuwa atatoa tamko rasmi baadaye.
Matukio ya makanisa kuchomwa yameshamiri katika Manispaa ya Bukoba, ambapo hili ni tukio la sita la kuchoma moto nyumba za ibada kwa kipindi cha mwaka mmoja.
NA JAMII FORUM

No comments