Header Ads

Magufuli Azomewa Jijini Mbeya.....Wananchi Wasema Wanamtaka Lowassa. Hapa kuna Video Mbili


Katika  hali  isiyo  ya  kawaida,Mgombea  Urais  kwa  tiketi  ya  CCM, Dr. John Magufuli  jana alijikuta  katika  wakati  mgumu  baada  ya  kukutana  na zomea zomea  ya  kundi  la  vijana  waliovamia  msafara  wake  akiwa  njianI  kuelekea  Mbarali  na kuanza  kuimba wakidai  Lowassa  ndo  Rais  wao....Tazama  Video hii

Magufuli aliyewasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, mkoani Mbeya saa tatu asubuhi na kuanza safari ya kwenda Mbarali, alikabiliwa  na  zomea zomea hiyo katika eneo la Soweto na Uyole.

Wafuasi hao wa Chadema waliuzuia  msafara  wa  Magufuli huku wakionyesha alama ya  vidole viwili juu, huku wengine wakizungusha mikono kama ishara ya mabadiliko inayotumiwa na chama hicho na kuimba Lowassa! Lowassa! Lowassa!
 
Tazama Na Hii Video

Baada ya kuona hivyo, Dk Magufuli aliwaomba wana-Chadema hao wamchague ili afanye mabadiliko bila kujali itikadi za vyama vyao.

Alisema akichaguliwa kuwa rais ataufanyia mabadiliko mji wa Mbeya kuwa M4C, “Sasa itakuwa Mbeya for Change kuwa kituo cha mabadiliko”

“Nikiwa rais, nitakuwa rais wa wote, nitakuwa Rais wa CCM, CUF, Chadema na hata wasio na vyama.

“Chadema oyeeeee, people,s....” Dk Magufuli aliwasalimia wananchi hao kwa salamu inayotumiwa na Chadema, nao wakamwitikia kwa sauti ya juu, ‘power’.

Alisema anatambua kuwa Mbeya kuna wafuasi wa Chadema na kuwataka wafuasi hao kumpa kura ili awaletee maendeleo. Alisisitiza kuwa Serikali yake itahakikisha vijana wote wanapata ajira ili waweze kujitegemea.

“Chadema mnasema people’s power, basi mnipe hiyo power ili niwaletee maendeleo,” alisema mgombea huyo na kuendelea na safari yake kwenda Mbarali.

No comments