Header Ads

LOWASSA ASHINDWA KUHUTUBIA GEITA KUTOKANA NA UFINYU WA MUDA NA SPIKA DUNI.

HABARI & PICHA:Na Paul William 

Mgombea ubunge wa chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi(UKAWA) mheshimiwa Edward Lowassa,leo ameshindwa kuzungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano wa chama hicho Geita mjini,kutokana na ufinyu wa muda ambapo amewasili katika viwanja hivyo kwa kuchelewa akitokea wilayani chato.
Aidha maandalizi ya mkutano huo hayakuwa mazuri ambapo spika zilikuwa hazitoi sauti na pia zilikuwa chache.
Akiongea wakati wa kufunga mkutano huo mwanasheria  wa chadema Tundu Lissu  ameahidi kurudi tena Geita ambapo wataandaa mambo vizuri kauli ambayo imeungwa mkono na mheshimiwa Lowassa huku akiahidi endapo atapewa ridhaa na wananchi ya kuwaongoza atahakikisha kuwa wachimbaji wadogo wadogo wanapatiwa maeneo yao ya kuchimba pamoja na haki zao za msingi. Pia kuahidi kuanzisha benki maalumu kwa ajili ya wachimbaji wadogo.


                   Wananchi wa Geita wakimsubili kwa hamu mgombea urais kupitia ukawa.

 Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Bahati Bukuku pamoja na Frola Mbasha wakiwasili katika viwanja hivyo leo.

 Umati wa watu wakisubili ujio wa mheshimiwa Lowassa katika viwanja vya magereza Geita mjini.
 Kutokana na wingi wa watu kuna baadhi ya watu walizidiwa na joto,kukosa pumzi na kupoteza fahamu ambapo vumbi pia kutajwa kuwa sababu.

 Mbunge wa Nyamagana Hainess Kiwia akiongea na wananchi kabla mheshimiwa Lowassa hajawasili katika viwanja hivyo.
Mgombea ubunge jimbo la Geita kupitia chama cha demokrasia na maendeleo Rodgers Ruhega  akiongea na wananchi kabla mheshimiwa Lowassa hajawasili katika viwanja hivyo.
                      Huduma ya kwanza ikitolewa kwa mtu aliyepoteza fahamu.
 Mgombea urais kupitia UKAWA Edward Lowassa akiwasili katika viwanja vya magereza mjini Geita ambapo hata hivyo amefika kwa kuchelewa akitokea wilayani Chato.



                                  Mheshimiwa Lowassa akiwasalimia wananchi.
                                                                    Meza kuu.

No comments