Header Ads

3 WAFARIKI NA WENGINE 51 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI GEITA.





Watu 3 wamefariki dunia  na wengine  51 kujeruhiwa katika ajali ya basi   aina scania kampuni ya shelatoni lenye namba za usajili T 138 AVD katika eneo la nyatorotoro mjini geita lililokuwa likitokea Runzewe wilayani bukombe mkoani hapa likielekea jijini mwanza.

Wakizungumza na PAUL BAHEBE,baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa walisikia mlio wa  tairi kupasuka na baada ya hapo waliona basi likiyumba na kuacha njia kisha kumgonga mwendesha pikipiki maarufu kama  boda boda pamoja na mwendesha baskeli.


Kwa upande wao baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa  katika hosptali ya wilaya ya geita,wamesema  kuwa walicho kiona ni  dereva  akimkwepa mwendesha pikipiki, (bodaboda)baada ya hapo hawakujua kilicho endelea hadi gari hilo linadondoka chini.

Nae mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya geita,Dr,Adam Sijaona, amethibitisha  vifo  hivyo na kupokea maiti 3 na majeruhi 51 ambao wemelazwa katika hosptali hiyo na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa,joseph konyo,amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba chanzo cha ajali ni kupasuka kwa tairi ya mbele upande wa kushoto hali iliyopelekea basi hilo kuyumba na kudondoka.

 Aidha joseph konyo ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo mbali mbali vya usafiri kuwa na desturi ya kuvikagua na kuvifanyia  marekebisho baadhi ya vitu ambavyo vinaonekana kuchakaa ili kuepukana na ajali za mara kwa mara.

No comments