WANAFUNZI WA KIKE WAHUDUMIWA NA WALIMU WA KIUME BUMANJI-GEITA.
Ruthian Bundala kaimu mkurugenzi
halmashauri Geita.
Na Joel Maduka
WANAFUNZI
WA KIKE WA SHULE YA MSINGI BUMANJI ILIYOPO KATA YA SHILOLELI WILAYA NA MKOA WA
GEITA WAMEIOMBA SERIKALI NA WIZARA YA
ELIMU KUPELEKA WALIMU WA KIKE SHULENI HAPO KWANI WAMEKUWA WAKIPATA SHIDA
PINDI WANAPO KUWA KATIKA MZUNGUKO WA MWEZI.
WAKIZUNGUMZA
NA STORM FM KWA NYAKATI TOFAUTI WANAFUNZI WA SHULE HIYO WAMESEMA KUWA WANAPOKUWA WAKIPATA MATATIZO YA KIKE WANAKOSA MWALIMU
AMBAYE ATAWAHUDUMIA HALI AMBAYO HUPELEKEA WAKATI MWINGINE KUHUDUMIWA NA WALIMU WA KIUME.
KWA
UPANDE WAO WALIMU WALIOPO SHULENI HAPO WAMESEMA KUWA KUTOKANA NA TATIZO LA
KUKOSEKANA KWA WALIMU WA KIKE WAMEKUWA
WAKIPATA SHIDA YA KUWAHUDUMIA WANAFUNZI
WA KIKE HALI AMBAYO INAWALAZIMU MUDA MWINGINE KUWACHUKUA WAKE ZAO NA
KUJA KUTOA HUDUMA KWA WANAFUNZI HAO.
KAIMU
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MKOA WA GEITA , RUTHIAN BUNDALA,AMESEMA KUWA HALMASHAURI
HIYO IPO KATIKA JITIHADA ZA KUHAKIKISHA KUWA WANATATUA SUALA LA WALIMU WA KIKE
KUTOKUFIKA SHULE ZA VIJIJINI NA UHABA WA
WALIMU WA KIKE SIO SHULE HIYO TU KWANI SHULE NYINGI ZINACHANGAMOTO HIYO.
SHULE
YA MSINGI BUMANJI INAWANAFUNZI 503 NA
WALIMU 8,AMBAO WOTE NI WAKIUME,IDADI YA WASICHANA KUANZIA DARASA LA KWANZA HADI LA 7 NI 209 NA
WAVULANA NI 250 NA UPANDE WA WANAFUNZI AWALI
NI 43.
Post a Comment