Header Ads

VIDEO:ONA WAZIRI ALIVYORUSHA NGUMI KISA KUKATWA KURA ZA MAONI.


Wakati mwingine nawaza nashindwa kupata jibu,mababu zetu walipigana ili kuondokana na dhuluma za wakoloni,ubaguzi na unyanyasaji.Wengi walikuwa tayari hata kufa kwa ajili ya nchi zao mfano mzuri ni ule wa kina MKWAWA na wengine ambao hawakukubali uonevu wa aina yoyote.
Ninachokijua mimi mtu yeyote anayekuwa na wadhifa fulani yupo pale kwa niaba ya watu wengine,tunateua na kuchagua wawakilishi wetu bungeni ili kwenda kutusemea isingekuwa rahisi kwetu sote kwenda bungeni kila mmoja wetu kutoa kero yake.

Kiongozi ni mtu tuliyemwamini atangulie mbele kutuonyesha  njia,si kwamba sisi hatuoni hiyo njia,kwa hakika naomba nikinzane na kauli yangu mwenyewe kuwa kumwita KIONGOZI si sawa,tena haya majina ndio yanayowapa kiburi na kujiona wamesha maliza maisha yote na kusahau kuwa siku moja watakufa na miili kuwa chakula cha funza!Hakika nifikapo hapo sioni thamani ya mwanadamu na kujifanya yeye ni yeye nakutowajali wenzake.

Pengine ukajiuliza kwanini nimeandika yote haya tena wakati mwingine kwa maneno makali kidogo,ndugu zangu wenyewe sote tunashuhudia kinachoendelea wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu 2015.

Viongozi wetu tuliowapenda,kuwaheshimu na wengine kuwaamini leo ndio wanaoongoza kurushiana ngumi hadharani tena bila aibu kisa KUKATWA katika kura za maoni!Hivi wewe unayerusha ngumi ilikuwa bahati mbaya/kuonyesha kuwa na wewe ulienda china au nini hasa?
Kama mnagombana na kurushiana maneno ya AIBU hata kuyatamka nahisi kichefuchefu,swali langu je mnataka kwenda kututetea wananchi au kujaza matumbo yenu?AIBU YENU JAMANI!
Ikiwa wananchi wameamua upumzike kinachokufanya upigane ni nini?tena cha ajabu huyo mwenzako aliyeshinda kura za maoni ni mwanachama mwenzako katika chama kimoja.!
Wito wangu kwa Watanzania wenzangu "sisi ni wamoja tumeishi kwa umoja,upendo na amani kama ndugu kwa zaidi ya karne sasa tusikubali wanasiasa wenye uchu na madaraka,na masilahi yao binafsi kutuvuruga kwa namna yoyote ile"Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania.

PAUL BAHEBE

No comments