MANGOCHIE:KUPIMA AFYA NI SUALA LA MSINGI.
Omar Mangochie mkuu wa wilaya Geita.
Wananchi mkoani Geita wameaswa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara,na kuacha tabia ya kusubiri hadi waugue ndipo waende kupima.
Akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Geita katika zoezi la kupima magonjwa yasiyoambukiza,mkuu wa wilaya ya Geita Omary Mangochie amesema kuwa suala la kupima afya ni suala la msingi kwani mtu anapopima huweza kujua bayana nini hasa kinachomsumbua.
Naye kwa upande wake afisa mahusiano wa mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) Bwana Manase Ndoloma amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyoambukizwa yanaongezeka kwa kasi kubwa hali ambayo hupelekea watu kuugua bila ya kujitambua kile kinachowasumbua.
Post a Comment