DAR YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA DUNIANI.
SIKU ya kimataifa ya vijana duniani imeadhimishwa leo jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Gabriel Ole Sante viwanja vya Mnazi Mmoja Dar.
Maadhimisho hayo yameanzia Shule ya Sekondari ya Jangwani na kumalizika katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo yaliongozwa bendi ya jeshi la polisi (Brass Band).
Vijana wengi walijitokeza kuadhimisha siku hiyo kutoka shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yalikuwa na kaulimbiu ya ‘Ushiriki wa Vijana Kwenye Maamuzi ya Maendeleo’ ambapo mgeni rasmi alisema vijana wanapaswa kusimama imara katika shughuli za kuleta maendeleo ili kutimiza ndoto zao katika ujenzi wa taifa. GLOBAL PUBLISHERS
Post a Comment