MAANDALIZI YA IDD GEITA, POLISI KUIMARISHA ULINZI.
kamanda konyo
JESHI
LA POLISI MKOANI GEITA LIMEWATAKA WANANCHI KUSHEREKEA SIKU KUU YA IDDY
KWA AMANI NA UTULIVU WAKATI WOTE WA SHEREHE HIZO,AMBAPO KITAIFA ZITAKUWA MKOANI GEITA,HUKU MAKAMU WA RAIS DK.MOHAMMED GHARIB BILALI AKITARAJIWA KUHUDHURIA SHEREHE HIZO NA VIONGOZI WENGINE WA DINI NA SERIKALI.
AKIZUNGUMZA
NA PAUL BAHEBE BLOG,KAMANDA WA MKOA JOSEPH KONYO ,JUU YA UTULIVU WA WANANCHI KATIKA
KIPINDI CHA SHEREHE ZA IDDY.
KAMANDA
KONYO,AMESEMA KUWA NI VYEMA KWA WANANCHI KATIKA KIPINDI HIKI KUWA WAANGALIFU
NA KUSHEREHEKEA KWA AMANI NA KUACHANA NA MAMBO AMBAYO YATAKUWA YANAONYESHA
VIASHAILIA VYA UVUNJIFU WA AMANI.
AIDHA KAMANDA KONYO,AMEWATAKA WAZAZI KUWA
WAANGALIZI WAZURI KWA WATOTO NA KUWA NA UKARIBU HUSUSANI MAENEO YA BARABARANI.
JESHI
LA POLISI MKOANI GEITA LIMEJIPANGA VYA KUTOSHA MKOANI HAPA KWA RAIA YEYOTE ATAONEKANA KUVUNJA AMANI ,ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA IKIWA NI PAMOJA
NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.PAUL BAHEBE
Post a Comment