KAGAME CUP KUENDELEA LEO.
Michuano ya kombe la Cecafa Kagame Cup inayoendelea kutimua vumbi nchini Tanzania itaendelea kupigwa leo kwa michezo ya kundi A.
Katika mchezo wa kwanza utakaochezwa majira ya saa nane kwa saa za Afrika mashariki utazikutanisha timu vinara za kundi hilo Khartoum ya Sudan dhidi Gor Mahia ya Kenya wote wakiwa na alama sita ila Khartoum wakiongoza kwa idadi ya mabao.
Mchezo wa pili utakaopigwa saa kumi jioni utakuwakutanisha ndugu wawili Yanga ya Tanzania bara dhidi ya Kmkm ya Visiwan Zanzibar ambapo wote wana pointi tatu hivyo ushindi ni lazima kwa kila timu ili kutengenezea nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali.
Timu ya Telecom ya Djibouti iliyoko kundi hili imekwisha yaaga mashindano hayo baada ya kutoambulia pointi hata moja katika michezo mitatu iliyocheza.
Post a Comment