FEDHA ZA MANJI BADO ZACHUNGUZWA
Mfanyabiashara Yusufu Manji.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema linaendelea kufanya uchunguzi wa mamilioni ya fedha zilizokamatwa katika Hoteli ya St. Gaspar mjini Dodoma, zinazodaiwa kuwa zilitolewa na Mfanyabiashara Yusufu Manji, kwa nia ya kuwahonga waliokuwa wajumbe wa vikao vya maamuzi vya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime, jana alisema kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo na kuahidi kutoa taarifa kamili kwa vyombo vya habari.
"Bado tunalishughulikia, subirini taarifa ikikamilika, tutaitoa tu, msiwe na wasiwasi wala msisababishe, tufanye kazi kwa shinikizo, " alisisitiza Kamanda Misime, wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jioni.
Kwa upande wake, Kamanda wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa(Takukuru), Emma Kuhanga, alisema kuwa pamoja na kupata taarifa kuhusiana na tukio hilo kutoka kwa vyanzo mbalimbali, hawako tayari kulizungumzia kwa sababu linachunguzwa na Jeshi la Polisi.
Kuhanga alisema wao polisi wanachunguza tukio hilo kwa kuwa maofisa wa taasisi yao (Takukuru) hawakuwapo kwenye eneo la tukio na kwamba kwa kawaida polisi pia hushughulikia makosa ya rushwa.
"Ikitokea ushahidi ukakamilika, kwakuwa sisi tuna prosecutor (mwendesha mashtaka) wetu, polisi wakiona umuhimu wa kuhamishia suala wanaloshughulikia ambalo linahusu rushwa, wanaweza kulihamishia kwetu kwa kufahamu kuwapo kwa chombo maalumu kinachoshughulikia makosa ya rushwa tu, " alisema Kuhanga.
Fedha hizo zilikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli hiyo iliyopo eneo la Kisasa, zikiwa mikononi mwa mfanyakazi wa Kampuni ya Quality Group (T), Amit Kevaramani, akiwa na hati ya kusafiria M1470774 ya nchini India.
Kiasi cha fedha kilichokamatwa ambacho hakijathibitika mara moja kinadaiwa kufikia Sh. 725,2050,000.
Inadaiwa kuwa fedha hizo zilikamatwa baada ya kuwapo kwa watu walioshtukia mwenendo wa mfanyakazi huyo wa kampuni ya Manji, aliyeonekana akihamisha mabegi makubwa mawili na kupeleka kwenye gari lililokuwa limeegeshwa nje ya hoteli hiyo likiwa aina ya Toyota Land Cruiser.
Katika hoteli hiyo ambayo kulikuwa na wajumbe wengi wa Mkutano Mkuu, na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM inadaiwa kuwa mamilioni hayo yalikuwa yanapelekwa kwa kambi ya mmoja wa wagombea watano waliopitishwa na Kamati Kuu wiki iliyopita kuwania kuteuliwa kuwa wagombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu. CHANZO: NIPASHE

Post a Comment