CHADEMA GEITA HAKUKALIKI BAADA YA MTIA NIA KUKATWA.
WAFUASI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)WILAYANI GEITA WAMETISHIA KUKIHAMA CHAMA HICHO ENDAPO MTIA NIA WA KITI CHA UBUNGE KUPITIA CHAMA HICHO BW RODGERS LUHEGA HATA PITISHWA KWENYE KURA ZA MAONI.
WAFUASI HAO WAKIZUNGUMZA NA STORM FM WAMESEMA KUWA KIONGOZI AMBAE WANAAMINI ATAONGOZA VIZURI NA KULETA MABADILIKO KATIKA MJI WA GEITA NI RODGERS NA KAMA LAITI CHAMA HICHO HAKITAMPITISHA MGOMBEA HUYO KUGOMBEA UBUNGE , WAKO RADHI KUKIHAMA CHAMA CHA CHADEMA.
AIDHA KWA UPANDE WAKE MTIANIA,BW RODGERS LUHEGA,AMEWATAKA WAFUASI HAO KUWA WAVUMILIVU KWANI KULA ZA MAONI KIKAWAIDIA ZINAWATOA WATU WATATU NA KUWAPELEKA KAMATI KUU AMBAPO HUJADILIWA NA KUTOA MGOMBEA MMOJA.
AKITOA MATOKEO YA UCHAGUZI WA KURA ZA MAONI , MSIMAMIZI WA UCHAGUZI HUO ,BW COSMAS SHIRATU AMESEMA KUWA JUMLA YA KURA ZILIKUWA 180 NA WAGOMBEA WALIKUWA SITA WALIOPITISHWA KUPELEKWA KAMATI KUU NI WATATU.
CHANZO/KURA ZA MAONI CHADEMA/JOEL MADUKA/24JULAI2015
Wafuasi wa Chadema wakipinga matokeo.
Post a Comment