ZAIDI YA WATU 500 WAJERUHIWA NA MOTO TAIWAN.
Zaidi ya watu 500 wamejeruhiwa kufuatia kutokea kwa mlipuko na moto kwenye bustani moja ya burudani nchini Taiwan.
Karibu watu wengine 200 walijeruhiwa vibaya kwenye ajali hiyo iliyotokea karibu na mji mkuu Taipei wakati kitu kisichojulikana kinachofanana na unga kililipuka kwenda hewani.
Baadhi ya watu wanaaminika kupumua unga huo hali iliyosababisha wapate matatizo mabaya ya kupumua.
Picha za video zilionyesha watu wakilia huku waokoaji wakiwabeba wale waliopata majeraha ya moto
Uchunguzi wa kubaini kilichosababisha moto huo unaendelea.na bbc
Post a Comment