WEMA SEPETU NA SABABU ZAKE KUWANIA UBUNGE,HAYA HAPA ALIYOSEMA.
"Nimezaliwa kwenye siasa, Marehemu baba yangu alikuwa ni mwanasiasa, mama yangu ni mwanasiasa mpaka sasa hivi ni Mwenyekiti wa Serikali za mitaa. Marehemu baba yangu aliwahi kuniambia kwamba anatamani niingie kwenye siasa, mwaka 2010 nilikuwa siko tayari.. nimejisikia vibaya baba yangu amefariki wakati sijaonesha kwamba ninaweza kufanya, nina uhakika kule aliko anajisikia fahari” Alisema Wema juzi akihojiwa kwenye kituo kimoja Runinga cha CLOUDS TV.
Kwanini kagombea Singida?; “Mama yangu ametoka Singida, nimeona hiyo ndio sehemu nzuri ya kwenda kugombea na huu ndio muda sahihi… nadhani ninaweza kujitolea kwa jamii yangu kwa sababu Singida ni nyumbani“>>> Wema Sepetu.
Kwanini kagombea Singida?; “Mama yangu ametoka Singida, nimeona hiyo ndio sehemu nzuri ya kwenda kugombea na huu ndio muda sahihi… nadhani ninaweza kujitolea kwa jamii yangu kwa sababu Singida ni nyumbani“>>> Wema Sepetu.
Akipata Ubunge nafasi ya kwanza ni yeye na wanawake; “Kipaumbele changu itakuwa ni wanawake, kwa sauti yangu na ushawishi wangu ninajua kwamba nitaweza”
Vipi akiangalia anaona upepo umekaa vizuri? “Upepo uko vizuri… Nilikuwa Singida wiki iliyopita na ninarudi wiki ijayo.. nitakuwa nafanya ziara ili wapate kuniona. Singida mimi ni maarufu sana kwa sababu ya mama yangu anatokea kule, kwa hiyo wanahitaji kumuona mtoto wao… Huwezi kujiwekea asilimia 100 kwamba utashinda lakini unatakiwa kuweka 75% kwamba utashinda… nafarijika kwa jinsi wanavyonipokea. Wasanii tuna nafasi nzuri kwa sababu tunafahamika” >>> Wema Sepetu.
Post a Comment