Header Ads

WADAU WA FILAMU WAIPONGEZA BODI YA FILAMU TANZANIA.

 

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya biashara ya DCB Bw. Samwel Dyano akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Balozi Paul Rupia hayupo pichana juzi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed iliyodhaminiwa na benki hiyo kwa lengo la kuhamasisha jamii kutumia huduma za kibenki katika kuyafikia mafanikio yao.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Balozi Paul Rupia akizungumza wakati wa  hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed juzi jijini Dar es Salaam.Filamu hiyo imetengenezwa na ya Kampuni ya Consnet Group Ltd ya jijini Dar es Salaam kufuatia udhamini wa DCB Benki ikiwa ni njia ya kujitangaza.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Consnet Group ambayo ndiyo waandaaji wa filamu ya Desire to Succeed Bw. Sanctus Mtisimbe (mwenye tai nyekundu) akiwatambulisha baadhi ya wasanii (wahusika) muhimu walioshiriki katika filamu hiyo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu hiyo iliyoambatana na futari chini ya udhamini wa Benki ya Biashara ya DCB.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akitambulishwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed iliyodhaminiwa na benki hiyo kwa lengo la kuhamasisha jamii kutumia huduma za kibenki katika kuyafikia mafanikio yao.
 Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed wakijitambulisha juzi jijini Dar es Salaam.Filamu hiyo iliyodhaminiwa na benki ya Biashara ya DCB.
Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo, msanii Rose Ndauka, Tito Mrisho Zimbwe na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB Balozi Paul Rupia wakionyesha DVD ya filamu ya Desire to Succeed juzi jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzinduliwa rasmi. Filamu hiyo imetengezwa na kampuni ya Consnet Group chini ya udhamini wa DCB Benki ikiwa ni njia ya kujitangaza kupitia ubunifu wa sanaa ya filamu.MICHUZI.

No comments