Header Ads

TATIZO LA KUZIBA MIRIJA YA UZAZI.

Kuziba kwa mirija ya uzazi huchukua asilimia ishirini ya tatizo la ugumba kwa mwanamke au mwanamke kupoteza uwezo wa kuzaa, pamoja na hizo sababu tatu, pia zipo sababu nyingine ndogo nyingi ambazo tutakuja kuziona kwa undani katika uchambuzi ujao.
Aina za uzibaji ni mirija kuziba upande wa mwishoni karibu na vifuko vya mayai ‘Distal tubal occlusions.’
Hali hii inahusiana kabisa na tatizo la mirija kuvimba au kujaa maji hali iitwayo kitaalamu Hydrosalpinx ambapo pamoja na mwanamke kushindwa kupata mimba, pia husumbuliwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa mara yanayosambaa kulia na kushoto.
Hali ya kuvimba kwa mirija au mirija ya uzazi kujaa maji husababishwa na maambukizi ya vimelea vya ‘Chlamydia trachomatics’.
Katika hali hii pia huweza kutokea hali ya kizazi na viungo jirani kushikamana hivyo mirija pia hushikwa na kuziba.
Hali hii ya kuziba mirija mwishoni husababisha sehemu ya mirija iliyo kama vidole iitwayo ‘fimbriae’ kugandamana na kusababisha kushindwa kuchukua yai lililopevuka na kuliingiza katika mirija tayari kwa kutungisha mimba.
Tatizo hili linapotokea, sehemu nyingine ya mirija inakuwa wazi au nzima. Mrija unaweza kuziba katikati ‘midsegment’ ambapo sababu kubwa inaweza kuwa mrija kufungwa au kukatwa kama njia ya kufunga uzazi. Mrija unaweza kuziba mwanzoni na sababu kubwa ni maambukizi kwenye kizazi kutokana na utoaji au kuharibika mimba na maambukizi mengine sugu ya kizazi.
Pata dondoo za afya za madaktari bingwa kwenye simu yako ya Vodacom bure: Tuma DAKTARI kwenda 15542.GLOBAL PUBLISHERS.

No comments