Header Ads

MAUJANJA.

KUJULIANA hali ni jambo la muhimu kwa binadamu, niwafahamishe mashoga zangu kuwa hali yangu na familia ni njema hakuna mushikeri wowote juu ya afya zetu, mategemeo yangu kuwa nyie pia ni wazima na mambo yenu yanasonga kama kawaida.
Kabla sijaianza mada ya leo inayosomeka “Si lazima mumeo akuanze mnapokuwa faragha” niwape pole ndugu zangu ambao mko kwenye mfungo wa Ramadhani, leo ni siku ya kumi na tatu mkiwa kwenye swaum Mungu awatie wepesi mmalize salama.
Nikiuliza mjitokeze mashoga ambao mna uwezo wa kuwaanza waume zenu muwapo faragha ni hakika yangu kuwa wengi wenu mtainamisha vichwa chini au kuangalia pembeni mkimaanisha ni vigumu sana kuonesha uhitaji kwa waume wenu.
Lakini niwaambie tu mashoga zangu hakuna kitu kizuri kinachoweza kumfurahisha mumeo kama kuonesha kuwa unahamu ya kukutana naye pale muwapo kwenye uwanja wenu wa kujidai.
Bila shaka anapofanya hivyo kwako unajisikia furaha eeh, unatambua ni kwa namna gani unahamasa hadi mumeo anakuwa na hamu ya kukutana nawe, sasa kama ilivyo kwako ndivyo inavyoweza kuwa kwa mumeo pia.
Jenga utaratibu hata bila kumwambia kuwa mtakuwa na zamu, kakuanza leo, wakati mwingine mkutanapo usisubiri tena hadi ‘kigogo wako’ akunyemelee ukiwa umejikausha ‘kau’, onesha kumhitaji zaidi, mfuate hadi mahali alipo  anza utundu wako uliojaliwa utamtia hamasa aelewe kuwa kazi anayoifanya si haba.
Shoga hata siku moja hutakiwi kuwa baridi chumbani, ikiwa unampango wa kudumisha ndoa moja ya sehemu muhimu kudumisha ni mahali hapo, ukiharibu mimi simo ‘habari ya mjini’ nimekupa.
Mwanamke shupavu hata siku moja si muoga, anajua anachokifanya usisubiri yakukute uanze kwenda kwa waganga, jenga ndoa kwa busara zako mwenyewe.
Leo nimemaliza tukutane Jumanne nyingine panapo majaliwa. 

No comments