Header Ads

MAKUMI WAHUKUMIWA KIFUNGO JELA NCHINI MISRI.

Makumi wahukumiwa kifungo jela nchini Misri

Makumi ya wapinzani wa serikali nchini Misri wamehukimiwa kifungo jela, kwa tuhuma mbalimbali. Jana Jumapili mahakama moja ya nchi hiyo iliwahukumu watu 47 kifungo cha miaka mitatu hadi 15 kwa kuhusishwa na faili la vitendo vya ukatili katika mkoa wa al-Sharqiyyah. 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri sanjari na kuthibitisha habari hiyo, imetoa onyo kali kwa wapinzani wa serikali juu ya kufanya maandamano yoyote sanjari na kuwadia tarehe 30 kulipojiri mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Muhammad Mursi.
 Kwa mujibu wa wizara hiyo, serikali itatumia mkono wa chuma kukabiliana na mkusanyiko wowote wa upinzani. Hii ni katika hali ambayo Harakati ya Ikhwan al-Muslimiin iliyopigwa marufuku nchini humo, imeitisha maandamano makubwa katika maeneo yote ya taifa hilo dhidi ya serikali inayoongozwa na majenerali wa jeshi.
 Itakumbukwa kuwa, tarehe 30 mwezi Juni mwaka 2013, Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Ulinzi na Kamanda Mkuu wa vikosi vya taifa, alimuuzulu rais aliyechaguliwa na wananchi, Muhammad Mursi na kisha kumfunga jela.
 Kufuatia tukio hilo, maelfu ya wafuasi wa rais huyo walianzisha wimbi la maandamano wakitaka kurejeshwa madarakani rais huyo, suala ambalo limekuwa likikabiliwa na mkono wa chuma wa serikali na kupelekea mauaji ya kila mara nchini humo. ISR

No comments