Header Ads

KINANA KUMALIZA ZIARA YAKE NCHI NZIMA JIJINI MWANZA LEO.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo atahutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye viwanja vya Furahisha na kurushwa live katika vituo vitatu vya televisheni vya Star Tv, TBC na ITV.
Mkutano huu ndio utakuwa mkutano mkubwa wa kuhitimisha ziara za Katibu Mkuu nchi nzima alizoanza miaka miwili iliyopita.

Katibu Mkuu katika ziara zake ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
 Maandalizi ya kufunga vifaa vya sauti yakiwa yamekamilika kwenye uwanja wa Furahisha.

 Katibu w NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihakikisha kila kitu kipo sawa.
 Sauti zikijaribiwa
 Malikia wa Mipasho nchini Hadija Kopa (kulia) akiwa jukwaani na wasanii wa TOT Taarab tayari kwa maandalizi ya mwisho.
 Wanamuziki wa bendi ya TOT wakijaribu vifaa vyao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu gitaa wakati wa majaribio ya bendi ya TOT,kulia pichani ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu.

No comments