ZITTO AMPONGEZA HALIMA MDEE KWA KUCHAGULIWA UWAZIRI KIVULI.
Kambi rasmi ya upinzani bungeni, imetangaza baraza lake la mawaziri kivuli ambalo Chama cha ACT Wazalendo, chenye mbunge mmoja, Kabwe Zitto, ndicho hakikuingizwa kwenye baraza hilo. Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe alitangaza jana bungeni baraza hilo.
Chadema chenye wabunge wengi katika kambi hiyo, kina mawaziri vivuli wengi ikilinganishwa na vyama vingine na wakati huo huo, kina wizara nyingi ambazo kinaongoza peke yake kwa maana ya kuwa na mawaziri na naibu mawaziri vivuli.
Mbowe alisema idadi ya wizara alizotangaza inafanana na ya wizara za Serikali ya Awamu ya Tano ambazo zipo 19.
Hata hivyo Zitto hajazungumzia lolote kuhusiana na suala hilo mbali na kuonekana kuwapongeza baadhi ya walioteuliwa.
Kupitia account yake ya Twitter Zitto amempongeza mmoja kati ya wabunge wa UKAWA Halima Mdee kwa kuteuliwa kuwa Waziri kivuli wa Fedha na Mipango.
Hongera sana dada yangu @halimamdee kuteuliwa kuwa Waziri Kivuli Fedha na Mipango. Nitakupa Ushirikiano katika kuisimamia Serikali
@zittokabwe asante sana bro.... nakutegemea sana kiushauri,mwongozo na uzoefu. Tuko pamoja sana.
Post a Comment