Waziri Mbarawa Awakamua MAJIPU Wakurugenzi TCRA na TEMESA.
Waziri wa Ujenzi wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, kusitisha mara moja mkataba wa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nzagi, kwa kushindwa kusimamia ufungwaji wa kifaa cha kufuatilia mapato ya simu ya ndani katika mitambo ya kuchunguza mapato katika mitandao ya simu (TTMS).
Waziri Mbarawa amesema kutokufungwa kwa kifaa hicho kumeisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 400/= hivyo ameiagiza pia bodi hiyo ya TCRA kuwasimamisha kazi mara moja, Kaimu Mkurugenzi anayesimamia mfumo wa uhakiki na usimamiaji huduma za mawasiliano, mhandisi Sunday Richard na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Modestus Ndunguru ili kupisha uchugnuzi dhidi ya uhusika wao katika kusababisha kifaa hicho kutokufungwa.
Aidha, Waziri Mbarawa ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRCA, Ally Simba kwa kutokuwa makini katika utendaji huo huku akimwagiza kuhakikisha kuwa kifaa hicho kinafungwa ndani ya siku saba.
Profesa Mbarawa pia ametengua uteuzi wa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Umeme na Ufundi Tanzania (Temesa),Mhandisi Marcellin Magesa kwa kushindwa kusimamia matengenezo ya magari ya serikali, mitambo na vivuko.
Kadhalika, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa matengenezo ya magari ya serikali,Prisca Mukama na Meneja wa Karakana ya magari ya Serikali John Mushina ambao watapangiwa majukumu mengine.
Post a Comment